UFUKONI PRIMARY SCHOOL VISITATION

UFUKONI PRIMARY SCHOOL VISITATION

Taasisi Ya Women and Youth voice Foundation ametembelea Shule ya Msingi Ufukoni iliyopo Wilaya ya Kigamboni-Dar Es Salaam na kuwapa wanafunzi elimu juu ya ukatili wa kijinsia. Taasisi ya Women and Youth Voice Foundation imejikita katika kutetea haki za watoto wa kike na kiume,wanawake na vijana katika maswala ya kisheria na ukatili wa kijinsia.
Taasisi hiyo imeanza kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwenye shule ya msingi Ufukoni iliyopo Wilaya ya Kigamboni,lengo likiwa ni kuzifikia shule tano zilizopo ndani ya Wilaya ya Kigamboni, na mipango ni kuzifikia shule nyingi zaidi nchini Tanzania.
Licha ya mafunzo ya ukatili wa kijinsia,Taasisi pia iliwapa wanafunzi elimu ya kujitambua na kujiamini ili waweze kuzifikia ndoto zao. Idadi ya wanafunzi waliohudhuria mafunzo hayo ni 76,watoto wa kike 34 na wa kiume 42

View more images