KAMPENI YA KUTEMBELEA WATOTO YATIMA

KAMPENI YA KUVIFIKIA VITUO 200 VYA WATOTO YATIMA

Taasisi ya Women and Youth voice foundation imepanga kuvifikia vituo 200 vya watoto yatima kwa tanzania Bara na visiwani huku ikipanga kuanza na vituo 10 mkoa wa Dar es salaam.
Akizungumza January 9, 2022 katika kikao cha kwanza cha mwaka 2022, Mkurugenzi mkuu wa WYV, Mwanaisha mndeme alisema hatua hiyo ni miongoni mwa malengo ya taasisi kwa mwaka huu.
Alisema baada ya kuvifikia na kutoa msaada katika vituo hivyo, wataendelea na zoezi hilo kwa mikoa mingine ya jirani. "Lakini pia tutaangalia na uhitaji wa mkoa husika, kwa mikoa ambayo iko karibu tunaweza kuanza na Tanga au Morogoro,lakini kwa kushirikiana na maafisa maendeleo wanaweza kutusaidia kujua kuna uhitaji kiasi gani kwenye eneo hilo, " Ameongeza mwanaisha.
Amesema lengo lingine ni kuhakikisha wanatoa elimu ya kisheria bure kwa wenye uhitaji na katika kufanikisha hilo wamepanga kufanya makongamano na warsha ili kutimiza lengo hilo. "Lengo ni kuwafikia watoto wa kike na kuwashauri na elimu kuhusu unyanyasi wa kijinsia,kujiamini na kujitambua, pia elimu ya kisheria bure tutaangalia makundi yote yenye uhitaji maalumu," alisema Mwanaisha.

Featured Causes