YOUNG WOMEN DONATION
Women and Youth Foundation has bought women sanitary pads as a preparation on the event to educate women on their rights
Taasisi ya Women And Youth Voice Foundation (@wyvfoundation) imetembelea Makao makuu ya kulea watoto yatima Kibada
( Hisani Orphanage Centre) kilichopo Kata ya Kibada, Jimbo la Kigamboni, Mkoa wa Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisis hiyo Mwanaisha Mndeme Ameongea na watoto wa kike wa kituo hicho na kuwapa elimu
juu ya ukatili wa kijinsia na kujitambua. Taasisi hiyo pia imeweza kuwapa #LavySanitaryPads wasichana hao..
Wasichana wa kituo hicho wataendelea kupata #lavypads kila mwezi kutoka Taasisi hiyo kama mchango wao katika kuhakikisha wasichana hao wanapata hitaji la Pedi kila mwezi.
Lengo la Taasisi hiyo ni kuwafikia watoto wa kike kwenye vituo vya watoto yatima 200 nchi nzima na kuhakikisha wanawapatia Pedi kila mwezi.
Licha ya kuongea na watoto wa kike wa kituo hicho Cha Hisani Orphanage Centre, pia wameweza kuwapatia baadhi ya mahitaji kama mchele, unga, mafuta, sabuni.
wyvfoundation ni Taasisi isiyo ya kiserikali iliyojikita katika kuwawezesha watoto wa kike,wanawake na vijana waweze kufikia malengo yao ya kuishi,ushirikishwaji na maendeleo nchini Tanzania.