
YOUNG WOMEN DONATION
Women and Youth Foundation has bought women sanitary pads as a preparation on the event to educate women on their rights
TAASISI ya Women and Youth Voice Foundation, imeanzisha program ya kutoa elimu kuhusu sheria na ukatili
wa kijinsi kwa wanafunzi wa shule za msingi wilayani Kigamboni mkoani Dar es Salaam. Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Mwanaisha Mndeme, ambapo aliweka bayana kuwa lengo kuu la wao
kuanzisha taasisi hii ni kusaidia jamii ya Kitanzania kupata ufahamu wa masuala ya kisheria na
ukatili wa kijinsia.
Mndeme amesema kwa siku za karibuni kasi ya jamii kutojua sheria na matukio ya ukatili wa kijinsia
yamekuwa yakiongezeka hivyo njia sahihi ya kukabiliana na changamoto hiyo ni kutoa elimu kuanzia ngazi
ya shule za awali, msingi na sekondari. Mkurugenzi huyo amesema katika program hiyo wanatarajia kufikia
wanafunzi wa jinsi zote katika shule zaidi ya tano wilayani humo na kwamba mipango yao ni kuwafikia Watanzania wote.
“Tunatarajia kuanzia wiki ijayo, tutaanza kutekeleza program yetu ya kutoa elimu kuhusu masuala
ya kisheria na ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule takribani tano ambazo ni Kigamboni,
Ufukoni, Vijibweni, Kisiwani na Mji Mwema,” amesema.
Amesema imani yao kupitia mafunzo hayo kwa wanafunzi wa shule za msingi, wataweza kubainisha mitazamo
kwa kundi hilo ambalo limekuwa likikumbana na changamoto hasa ya ukatili wa kijinsia. Mkurugenzi huyo
amesema katika mafunzo hayo watashirikiana na maofisa maendeleo ya jamii kutoka halmashauri jambo ambalo
litaongeza uzito. Mndeme amesema pia watatumia mafunzo hayo kuwapa wanafunzi motisha na kujiamini ili
waweze kutimiza ndoto zao, ambapo wengi wao zinaishia njiani.
“Kuna changamoto kubwa ya makuzi kwa watoto wetu, hivyo naamini kupitia program hii tutaweza kuwafanya
wanafunzi kuishi katika ndoto zao,” alisema. Aidha, mkurugenzi huyo alitoa rai kwa wadau mbalimbali
kuwapa ushirikiano ili waweze kufikia malengo yao ya kufikia kila pande ya nchi hasa vijijini ambapo
changamoto ya masuala ya sheria na ukatili wa kijinsia vipo. Mndeme amesema taasisi yao inaamini
iwapo kila mdau atashiriki katika utoaji elimu kuhusu sheria na madhara ya ukatili wa kijinsia ni dhahiri kuwa jamii itabadilika na kuishi kwa upendo na amani.